Maafisa wa usalama nchini Ivory Coast, wameitaka Serikali ya Mali kuwaachilia mara moja wanajeshi wake 49 waliokamatwa Juni 10, 2022 katika uwanja wa ndege wa Kimataifa jijini Bamako, huku ikikanusha tuhuma kuwa walikuwa ni mamluki.

Serikali ya Ivory Coast, imesema wanajeshi hao walisajiliwa katika kikosi kazi cha Jeshi la Ivory Coast, na walikuwa nchini Mali kama sehemu ya ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa.

Awali, msemaji wa Serikali ya Mali, Kanali Abdoulaye Maiga aliwashutumu kwa kuwa kinyume cha sheria katika eneo la kitaifa la Mali huku wakiwa na silaha na zana za vita, bila taarifa yeyote na kupata idhini toka mamlaka za nchi hiyo.

Wanajeshi wa Ivory Coast wakati wa uzinduzi wa chuo kipya cha kimataifa kitakachotoa mafunzo kwa wataalamu wa usalama wa raia na maafisa wa kijeshi katika mapambano dhidi ya ugaidi, huko Jacqueville, Ivory Coast Juni 10, 2021 kabla ya kukamatwa.

Wanajeshi hao walikuwa wakitakiwa kufanya kazi katika shirika la Sahelian Aviation Services, ambayo ni Kampuni binafsi iliyopewa kandarasi na Umoja wa Mataifa, kama ambavyo iliarifiwa na serikali zote mbili.

Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa, Farhan Haq amesema kikosi hicho si sehemu rasmi ya ujumbe wao wa kulinda amani nchini Mali, lakini kimetumwa na nchi zinazochangia Wanajeshi kusaidia vikosi vyao, kitu ambacho ni kawaida katika misheni za kulinda amani.

Serikali ya Mali ilisema inakusudia kusitisha shughuli za ulinzi wa Huduma za Usafiri wa Anga za Sahelian na vikosi vya kigeni na itawataka waondoke katika eneo la Mali na kulitaka Shirika la ndege la Sahelian Aviation Services kuanzia sasa kukabidhi majukumu yake kwa vikosi vya ulinzi na usalama vya nchi hiyo.

Wanajeshi wa Mali.

Mali imekabiliwa na mvutano wa hivi karibuni na jumuiya ya kimataifa na Umoja wa Mataifa, huku Serikali ya mpito ya nchi hiyo ikithibitisha kuwa haitaidhinisha ujumbe wa Umoja wa Mataifa kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu unaoendelea nchini Mali.

Suala hili pia litaendana na tukio la kijiji kidogo katikati mwa nchi ya Mali ambapo jeshi lake linashutumiwa na makundi ya kutetea haki za binadamu kwa mauaji ya zaidi ya raia 300 huku Aprili, 2022 pia Ufaransa ikitangaza kuondoa vikosi vyake vilivyotumwa karibu muongo mmoja uliopita kusaidia kupambana na waasi wenye itikadi kali.

Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara

Ndege zisizo na rubani kupima ardhi Nchini
Wachezaji Simba SC na Young Africans wakutana JKCI kupima Moyo, Damu