Meneja wa klabu bingwa duniani Real Madrid  Zinedine Zidane, bado hajakata tamaa ya kuona beki wa pembeni kutoka nchini Austria na klabu ya Bayern Munich  David Olatukunbo Alaba, akitua Estadio Santiago Bernabeu.

Beki huyo amekua katika mipango ya usajili wa meneja huyo kutoka nchini Ufaransa tangu mwanzoni mwa msimu huu, lakini adhabu inayoikabili Real Madrid ya kutosajili wakati wa majira ya baridi (Januari 2017) imepunguza mbio za Zidane.

Zidane ameshakutana na rais wa Real Madrid Florentino Perez, na kumueleza dhamira yake kuhusu Alaba na amemtaka kumsajili kwa namna yoyote ile itakapofika mwishoni mwa msimu huu.

Endapo mipango ya Zidane itakaa kwenye mstari, Real Madrid watalazimika kulipa Euro milioni 65 kama ada ya uhamisho wa beki huyo mwenye umri wa miaka 24.

Usajili wa Alaba unathibitisha kuondoka kwa beki wa pembeni wa Real Madrid Fábio Alexandre da Silva Coentrão, ambaye alipelekwa kwa mkopo AS Monaco mwanzoni mwa msimu huu.

Pia usajili wa Alaba unatarajiwa kuleta changamoto kwa beki wa kushoto klabuni hapo Marcelo.

VPL: Mechi 14 Za Funga Mwaka, Mbili Kufungua Mwaka
Sallam aelezea collabo mpya ya Diamond, Rick Ross na Rihanna