Mkali wa ‘Always On Time’, Ja Rule amejibu tetesi zilizoenea kuwa 50 Cent anapanga kununua haki zote za albam yake.

Imeelezwa kuwa 50 anatafuta namna ya kununua Master CD ya albam hiyo ili awe mwenye haki ya kuamua kufyatuliwa kwa nakala na nyimbo.

Hata hivyo, Ja Rule amezifyekelea mbali tetesi hizo akieleza kuwa amejipanga vizuri na kwamba jaribio hilo kamwe halitawezekana.

Kiongozi huyo wa Murder Inc, ametumia mtandao wa Twitter kumjibu 50, akichelekea na kueleza kuwa rapa huyo hawezi kununua haki zake (Masters) kwakuwa yeye mwenyewe ndiye anayezimiliki.

Wiki chache zilizopita, 50 Cent alizua gumzo baada ya kudai kuwa amenunua tiketi 200 za mbele za tamasha la Ja Rule, ili nafasi zote za mbele zibaki wazi wakati rapa huyo atakapokuwa anatumbuiza.

Bifu kati ya 50 Cent na Ja Rule lina umri wa takribani miaka 15 hivi sasa. Bado kiongozi huyo wa G-Unit hajamjibu Ja Rule.

Solari: Ninaisaidia Real Madrid, sitafuti cheo
Suala la Gesi na Mafuta lamuibua Maalim Seif

Comments

comments