Hatimaye Ja Rule amejibu mapigo ya 50 Cent mtandaoni baada ya rapa huyo kumvuruka kwa kipindi cha wiki mbili mfululizo.

Pigo la mwisho la 50 Cent kwa hasimu wake huyo ni pale alipotangaza kuwa amenunua tiketi 200 za siti za mbele za tamasha la rapa huyo litakalofanyika Novemba 9 mwaka huu, ili zibaki wazi.

Ja Rule ambaye ameonekana kuchukizwa na kitendo hicho cha 50, ameweka mtandaoni picha iliyohaririwa kwa teknolojia (photoshop), ambayo inamuonesha kiongozi huyo wa G-Unit akiwa kwenye muonekano wa kike.

Rapa huyo aliambatanisha post hiyo na matusi kwa mkali huyo wa ‘Get the Strap’, ingawa wengi wamedai kuwa majibu hayo yako nje ya wakati huu na kwamba hayaendani na ubunifu anaoufanya 50 anapomshambulia.

Kutokana na maadili hatukuweza kuiweka post hiyo, ila unaweza kuona picha husika.

Kiongozi huyo wa Murder Inc na mwenzake wa G-Unit walioanza kushambuliana tangu mwaka 1999, wakirushiana makombora kwenye nyimbo zao kadhaa.

Wawili hao wamewahi kuripotiwa kutaka kuzichapa kavukavu baada ya kukutana kwenye klabu moja ya usiku jijini New York.

Angela Merkel atangaza kuachia ngazi 2021
Video: Mtandao kuchafua vigogo wanaswa, Lissu, Zitto vigeugeu

Comments

comments