Mwenyekiti wa klabu ya Bournemouth Jeff Mostyn ameonyesha kupendezwa na huduma ya kiungo kutoka Uingereza na klabu ya Arsenal Jack Wilshere, aliyesajiliwa kwa mkopo mwishoni mwa mwezi uliopita.

Mostyn amesema tangu kiungo huyo alipojiunga na klabu ya Bournemouth, kikosi chao kimekua na mabadiliko makubwa katika safu ya kiungo na anaamini endapo watawasilisha maombi ya kusajili moja kwa moja hakuna litakaloshindikana.

Wilshere tayari ameshaitumikiwa Bournemouth katika michezo mitatu ya ligi kuu ya Uingereza na amekua mmoja wa watu wanaovutiwa na kiwango chake kila kukicha.

“Tunaweza kufanya hivyo, naamini hakuna litakaloshindikana kwa sababu Wilshere anahitaji kucheza kila juma kama ilivyo hivi sasa.

“Huenda ikawa wakati wowote wa usajili ima mwezi Januari ama mwishoni mwa msimu huu, tutajaribu kufanya hivyo na ninaamini tutafanikiwa.

“Niwe muwazi, kiwango cha Wilshere ni kikubwa na kinaonyesha kuisaidia klabu yetu.” Alisema Jeff Mostyn

Hata hivyo mpango huo wa Jeff Mostyn, huenda ukapingwa vikali na meneja wa Arsenal  Arsene Wenger, ambaye anaamini kumpeleka Wilshere kwa mkopo katika klabu ya Bournemouth ilikua ni moja ya hatua ya kutaka kulinda kipaji chake kwa ajili ya maisha yake ya baadae ndani ya washika bunduki wa kaskazini mwa jijini London.

Stephane Sessegnon Arejea Ufaransa
Matuta barabara kuu ni chanzo cha ajali, yaondolewe