Hatimae kiungo Jack Wilshere amefanikiwa kurejea kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England ambacho baadae mwezi huu kitacheza michezo dhidi ya Scotland na Hispania.

Kocha wa muda wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate ametaja jina la kiungo huyo kuwa miongoni mwa wachezaji aliowaita kikosini, baada ya kuridhishwa na uwezo wake ambao anauonyesha akiwa na Bournemouth iliyomsajili kwa mkopo akitokea Arsenal.

Kwa mara ya mwisho Wilshere aliitumikia timu ya taifa lake la England wakati wa fainali za mataifa ya Ulaya ((Euro 2016), na tangu alipoteuliwa kocha aliyetangaza kujiuzulu Sam Allardyce hakubahatika kuitwa kikosini.

Wachezaji wengine ambao wameitwa kwenye kikosi cha England baada ya kukosekana kwenye michezo ya mwezi uliopita ni mshambuliaji wa Spurs Hary Kane na beki wa Burnley Michael Keane.

Kikosi kamili cha England ambacho kitapambana na Scotland/ Hispania ni:

Makipa: Forster (Southampton), Hart (Torino), Heaton (Burnley);

Mabeki: Bertrand (Southampton), Cahill (Chelsea), Clyne (Liverpool), Jagielka (Everton), Keane (Burnley), Rose (Tottenham), Stones (Man City), Walker (Tottenham);

Viungo: Dier (Tottenham), Drinkwater (Leicester), Henderson (Liverpool), Wilshere (Bournemouth), Lallana (Liverpool), Lingard (Man Utd), Rooney (Man Utd), Sterling (Man City), Townsend (Crystal Palace);

Washambuliaji: Walcott (Arsenal), Kane (Tottenham), Rashford (Man Utd), Sturridge (Liverpool), Vardy (Leicester).

Fenerbahce: Robin van Persie Yupo Salama
Cristiano Ronaldo, Florentino Perez Wakubaliana