Kiungo wa klabu ya Arsenal Jack Wilshere amethibitisha ataachana na klabu hiyo mwishoni mwa mwezi huu, mara baada ya mkataba wake kufikia kikomo.

Wilshere ambaye ameachwa kwenye kikosi cha England kinachoshiriki fainali za kombe la dunia zinazoendelea nchini Urusi, ameandika katika ukurasa wake wa Instagram taarifa za kuondoka kwake.

“Nitaondoka Arsenal mwishoni mwa mwezi huu, nimejaribu kuzungumza na uongozi kuhusu mkataba mpya lakini hatujafikia muafaka, njia rahisi iliyobaki ni kuangalia maisha mahala pengine,” ameandika Wilshere mwenye umri wa miaka 26.

“Lengo langu kubwa lilikua ni kuendelea kuitumikia Arsenal ambayo niliipenda na ninaendelea kuipenda, lakini sina budi kuchukua maamuzi haya kutokana na hali halisi iliopo.” Aliongeza kiungo huyo

Wilshere alianza kuitumikia Arsenal mwaka 2008 akiwa na umri wa miaka 17, na mpaka msimu uliomalizika (2017/18), alikua ameshacheza micheza 200 katika michuano yote.

Katika muda wa miaka 10 aliokaa klabuni hapo, Wilshere aliwahi kutolewa kwa mkopo kwenye klabu za Bolton Wanderers na Bournemouth.

Habari kubwa katika magazeti ya leo Juni 20, 2018
Wanaopenda michezo ya 'Kompyuta' hatarini kuugua ugonjwa wa akili