Aliyewahi kuwa Miss Tanzania mwaka 2000 na kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss World, Jacqueline Ntuyabaliwe, mwaka 2015 alifunga pingu za maisha na mfanyabiashara mkubwa na maarufu Tanzania, ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya IPP Media, Dk. Reginald Abraham Mengi

Jacqueline siku ya leo akiwa anasherekea miaka mitatu ya ndoa yake ameandika ujumbe mzito kwa mume wake Regnard Mengi ambaye tayari amemzalia watoto.

Amesema ”You’re my everything,I couldn’t have asked for a better man to call my husband.Thank you for spending your life with me and thank you for a beautiful love.Happy Anniversary to us.❤🎊”.

Akimaanisha, Wewe ni kila kitu kwangu, siwezi kutaka mwanaume mwingine na kumuita  mume wangu. Asante kwa kutumia/kuishi maisha yako na mimi, asante kwa upendo wako mzuri. Heri ya siku ya maadhimisho ya ndoa yetu.

Jacqueline amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa instagram, huku maneno hayo yakiwa yameambatanishwa na picha mbili za kumbukumbu ya siku ya harusi yao.

Jacqueline na Mume wake Mengi walifanya sherehe hiyo nchini Mauritius, ambapo ilihudhuriwa na watu 50 tu ikiwa ni ndugu na marafiki wa karibu wa wawili hao.

Harusi yao ni moja kati ya harusi kubwa na za kifahari zilizowahi kufanywa na watanzania.

Mungu aibariki ndoa ya wawili hao, wakapate kuishi milele na kutenganishwa na kifo pekee.

China yathibitisha ziara ya Kim Jong Un, ajipanga kumuona Trump
Ndugu zangu siwaoni, sijui wametekwa- Hashim Rungwe

Comments

comments