Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jaffo, amewapa onyo Wakurugenzi wa halmashauri pamoja na makandarasi watakaoshindwa kutimiza agizo la  kukamilisha ujenzi wa madarasa na nyumba za waalimu katika mradi wa Mes Two ndani ya muda uliopangwa.

Aidha Jaffo amesema kuwa  uzembe wowote utakaosababishwa nao  Serikali itawashughulikia ikiwa ni pamoja na kuwapiga marufuku makandarasi kupewa kazi zozote.

Ameyasema hayo mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba za waalimu na madarasa katika kijiji cha Manzase Chamwino Mkoani Dodoma.

“Nilipita hapa hivi karibuni, lakini viongozi wa Halmashauri hawakuonyesha kuutilia mkazo mradi huu, hadi nilipoamua kuwapa muda wa siku kumi uwe umekamilika, wametekeleza agizo hilo”amesema Jaffo.

Ukaguzi huo unafuatia baada ya kushuhudia mkandarasi kuutelekeza  bila taarifa yeyote, hivyo kuwapa muda viongozi kuhakikisha unakamilika kwa kipindi kifupi.

Tanzania yachunguza madai ya Malawi kuwakamata wapelelezi wake
BoT yafafanua uvumi wa matumizi ya noti ya 500/-