Naibu Waziri ,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Seleman Jaffo ameshitushwa na madudu aliyoyakuta katika Hospitali ya  ya Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani na kuagiza kuundwa kwa kamati ya kuchunguza kitendo cha uongozi wa hospitali hiyo cha kutonunua dawa ilihali Serikali imesha toa zaidi ya shilingi milioni 200.

Jaffo amesema kuwa Serikali ilishatoa fedha za kununua dawa ili wananchi wapate matibabu,lakini anashangazwa na uongozi wa hospitali hiyo kukaa na fedha wakati wananchi wanakosa huduma ya matibabu, amesema utaratibu uliopo wa kisheria unawataka watendaji kuzirejesha fedha Serikalini kama hazikufanya kazi inayokusudiwa katika mwaka wa fedha.

Aidha,Jaffo ameongeza kuwa hospitali hiyo ina matatizo mengi yakiwemo ya uchakavu wa majengo kutokana na kutokufanyiwa ukarabati,licha ya uongozi kupatiwa fedha na Serikali .

Kwa upande wake Mganga mkuu wa hospitali hiyo,Paulina Mbezi amesema wanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa madawa katika hospili hiyo hali ambayo inasababisha wagonjwa kwenda kujinunulia dawa kwenye maduka ya watu binafsi.

 

 

Agizo la Waziri Mbarawa laanza kutekelezwa
Majaliwa atoa onyo kwa Madiwani na watumishi