Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleman Jafo amemuagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Joseph Nyamuhanga kumsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mji wa Tarime, Jumanne Yassin ili kupisha uchunguzi kwa kosa la kusafirisha mwili wa Mkuu Idara ya Maendeleo, Marehemu Emamanuel Joseph juu ya carrier.

Waziri Jafo amesema kuwa watumishi wote watakaobainika kuhusikana na uzembe huo, watachukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa Umma kwa watumishi.

Jafo amesema kitendo hicho ni kinyume na kanuni ya Q7(1-e) ya utumishi wa umma, mila na desturi za Watanzania.

Aidha, Jafo amewataka watumishi wa wa umma katika Tawala za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa kujenga tabia ya kuheshimiana, kupendana na kuaminiana wakati wote na kuthaminiana wakati wote wanapotekeleza majukumu yao.

Marehemu Emmanuel Joseph alifariki kwa ajali ya gari mkoani, Singida tarehe 10, Januari 2021.

Dkt. Mwinyi, Maalim Seif wawasili Chato
PICHA: Taifa Stars yaenda 'CHAN' kwa tabasamu