Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amelitaka Shirika la Chakula Duniani (WFP) kuendelea kutoa ushirikiano katika miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ili kuendelea kuboresha masuala ya Lishe katika jamii.

Ameyasema hayo wakati wa kikao na Binti Mfalme wa Jordan Sarah Zeid cha kujadili masuala mabalimbali yanayohusiana na Lishe sambamba na miradi inayofadhiliwa na fedha za Umoja wa Ulaya kupitia Shirika la chakula Dunia.

Jafo amewashukuru kwa ushirikiano wanaoutoa katika miradi mbalimbali ya Lishe na hakika wamekuwa na mchango mkubwa katika kuboresha Lishe Tanzania kwa kuwa Lishe ni suala endelevu na mtambuka.

‘Hatuwezi kufikia Taifa la Uchumi wa Kati endapo watu wetu hawatakuwa na lishe bora, ili watu wafanye kazi kwa bidii, waweze kuzalisha na kulipa kodi inavyotakiwa ni lazima wawe na Afya bora wakati wote hivyo kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha lishe bora ni vitu muhimu sana katika kufikia lengo la Kitaifa,”Amesema Jafo

Kwa upande wake, Binti Mfalme Sarah Zeid amesema kuwa amefurahishwa sana na utekelezaji wa miradi ya Lishe inayotekelezwa katika Halmashauri nne Nchini na ameridhishwa na matokeo aliyoayaona kupitia miradi ya wananchi, huku akiahidi kupitia Shirika la Chakula Duniani (WFP) kuendelea kutoa ushirikiano katika miradi mingine.

 

Video: Majaliwa atoa onyo kali kwa Maafisa Elimu
Lil Kim atangaza tarehe ya kushusha albam yake mpya