Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo, amemwagiza mkandarasi wa kampuni ya Chico, inayojenga barabara za urefu wa kilomita 52, kwa kiwango cha lami katika Mji wa kiserikali kukamilisha ndani muda huku akiridhishwa na kasi ya ujenzi.

Waziri Jafo ametoa kauli hiyo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kukagua ujenzi wa barabara hizo katika mji wa kiserikali Mtumba Jijini Dodoma kutokana kuwa nyuma ya muda.

Amesema ujenzi wa barabara hizo unataikiwa kukamilika kwa muda uliopangwa bila kuwepo kwa kiasingizo ya aina yoyote hivyo kamilisheni kwa haraka na ongezeni kasi ya ujenzi.

“Niwapongeze sana, baada ya kutekeleza agizo nililolitoa kabla ya kuvunjwa kwa baraza la mawaziri leo nimekuta kuna mabadiliko makubwa sana na kasi yenu ni ya kuridhisha hivyo basi nataka mradi huu ukiamilike katika muda uliopangwa na siyo vinginevyo,”amesema Jafo.

Aidha, amemtaka mkanadarasi huyo kuacha kutumia kisingizio cha kuadimika kwa saruji hivyo kupelekea kuchelewa kukamilika kwa mradi huo kwakuwa ni changamoto ambayo ipo kwenye baadhi ya maeneo mengi nchini.

“Kama hakuna saruji fanyeni kazi nyingine ambazo hazihitaji saruji kama uchimbaji wa mitaro lakini isiwe kama hakuna saruji basi na nyinyi mnakaa bila kufanya kitu chochote sababu mkifanya hivyo hamta kamilisha leo kwa mwenendo huu,”.amesisitiza Waziri Jafo

Pia, alimuagiza mkanadarasi huyo kuhakikisha anafanyakazi ya ujenzi wa barabara usiku na mchana ili kukamilika ndani ya muda uliopangwa na kueleza kuwa ameridhishwa na kasi.

Watatu mikononi mwa TAKUKURU kwa kosa la wizi wa dawa
Oldonyo Lengai yaibuka picha bora