Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Seleman Jafo ametoa muda wa miezi miwili kwa Wakuu wa Mikoa wote nchini kuanza kusimamia ujenzi wa miundombinu ya shule katika Mikoa yao.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake, Jafo amesema miundombinu hiyo itahusisha ujenzi wa vyumba vya Madarasa 478 na mabweni 269 ambapo kila bweni moja litachukua wanafunzi 80.

Amesema kuwa ni wajibu wa kila Mkuu wa Mkoa kusimamia kusimamia kwa dhati kazi ya ujenzi wa miundombinu ya Madarasa na Mabweni na kuhakikisha kuwa fedha zinazotolewa na Serikali zinaendana na majengo yatakayojengwa kama walivyokuwa wakifanya katika miradi ya afya na Elimu.

Aidha, amesema kuwa kuwa Serikali imeweza kuchagua shule 119 ambazo orodha itatolewa wakuu wa Mikoa hiyo wahakikishe wanasimamia kwa haraka zoezi la kubaini maeneo ya yatakapojengwa madarasa na mabweni, pia kusimamia uteuzi wa Kamati za Ujenzi na kuanza mchakato wa kuwatafuta wajenzi wa majengo hayo.

“Niwatake Wakurugenzi ambao wanatabia ya kusuasua utekelezaji wa mradi mbalimbali kuacha mara moja na katika jambo hili sihitaji masihara hata kidogo, Mamlaka za Serikali za Mitaa itakapo pokea fedha ihakikishe inakamilisha ujenzi huo haraka.” Amesema Jafo

Hata hivyo, amewaagiza Wakuu wa Mikoa wote ambao Halmashauri zao kazi ya Ujenzi wa Miundombinu ya Shule inaenda kufanyika kusimamia kwa nguvu mchakato wa kutafuta mafundi wa ujenzi wa majengo na kuhakikisha wanapatikana haraka ili kazi ianze mara moja baada ya kubainisha maeneo.

Video: Tatizo Watanzania tumezidi kujirahisisha- Dkt. Mwakyembe
Serikali eSwatini yawatoza wanaofunga ndoa na raia wa kigeni

Comments

comments