Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Selemani Jafo ametoa siku kumi kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma kuhakikisha anasajili mradi wa ujenzi wa machinjio ya kisasa ili uweze kupata cheti cha tathmini ya mazingira.

Waziri Jafo amesema hayo akiwa kwenye ziara yake mkoani Kigoma alipotembelea machinjio ya Manispaa hiyo, ambapo amesema endapo Manispaa itashindwa kusajili mradi huo wa machinjio ya kisasa kwa kipindi tajwa atasitisha ujenzi huo.

“Naagiza mradi huu usajiliwe mapema iwezekanavyo, na lengo la kufanya hivi si kupata cheti tu bali muhimu ni kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu masuala muhimu ya kuzingatia katika utunzaji na uhifadhi wa mazingira,”  amesema Jafo.

Aidha Waziri Jafo amewasihi kusajili mradi huo kwa njia ya mtandao ambapo amesema kuna wengi wamesajili lakini hajaona mradi huo kwenye usajili na kufikia tarehe Mei 25, 2021 wawe wamesajili.

Sambamba na hayo waziri Jafo amewataka wawekezaji kote nchini kusajili miradi yao ili iweze kukidhi vigezo vya kupatiwa cheti cha tathmini ya athari kwa mazingira kinachoainisha namna bora ya kupunguza madhara ya kimazingira yatokanayo na utekelezaji wa miradi.

Ukwaju unavyoondoa tatizo la nywele kutakati
NEC yasisitiza amani uchaguzi mdogo