Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  Suleiman Jafo amewashauri viongozi walioteuliwa na Rais Magufuli katika nyadhifa tofauti kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa, kwa kuheshimiana na kupeleka maendeleo katika maeneo waliyopewa dhamana.

Waziri Jafo amesema huu ni usajili wa dirisha dogo, hivyo ni wajibu wa kila kiongozi aliyeteuliwa kuhakikisha anakwenda kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kumuwakilisha Rais, na kuwatumikia watanzania.

”Sisi tuliopewa dhamana katika maeneo mbalimbali jukumu letu kubwa ni kwenda kumsaidia Mh. Rais tukifanya mambo ambayo sio sawa sawa tunamuangusha Rais wetu, imani yangu kila mtu katika nafasi yake  aende akafanye jambo ambalo litampa faraja Rais wetu, kubwa kila mtu amuheshimu mwenzie tutapata mafanikio makubwa sana” amesema waziri Jafo

”Mkuu wa Mkoa wa Arusha umepata fursa, Mh. Rais Amekuamini, Nenda kaishi vizuri na wasaidizi wako.’’

Aidha amewataka wakuu wa wilaya wanaofanya kazi ofisi moja na wakuu wa mikoa  kufanya kazi kwa ushirikiano na upendo na kuleta heshima kwa wananchi.

Corona: Wakenya wanavyolia na ugumu wa maisha kuliko madhara ya kiafya
Trump ataka upimaji corona upunguzwe kasi, adai unaongeza idadi ya visa