Wananchi Wilayani Kisarawe wamepongezwa kwa ushirikiano mkubwa katika ujenzi wa miundombinu ya elimu ikiwemo ujenzi wa madarasa, Ofisi za walimu, nyumba, pamoja na vyoo.

Pongezi hizo zimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Kisarawe ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Selemani Jafo, wakati akikagua mradi ya ujenzi wa madarasa wilayani kisarawe katika vijiji vya Mitengwe, Kitonga, Boga, na kwala.

Katika vijiji hivyo, Jafo alikagua ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa 15, Ofisi za walimu 4, pamoja na matundu ya vyoo 40 ambapo ujenzi wake unafanyika kwa bora unaotakiwa.

Kutokana na muamko mkubwa ulioonyeshwa na wananchi hao katika kushirikiana na serikali na viongozi walio wachagua akiwemo mbunge na madiwani wote wa kisarawe, Jafo amesisitiza wananchi wengine katika wilaya mbalimbali kushirikiana na serikali pamoja na viongozi wao ili kujiletea maendeleo.


Video: HATARI!! “Tulivunja shule baada ya kukosa hela, wazazi wangu walinifanyia kitu cha ajabu sana”

Gari la Lema lachomoka matairi, adai 'watu wasiojulikana’ wamehusika
Nash Mc awasili Uganda kuiwakilisha Tanzania katika sanaa na Hip Hop