Katika kuhakikisha kuwa kila mtumishi wa umma anatimiza wajibu wake, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Selemani Jafo amewataka watumishi wa halmashauri ya mji wa Tarime na Halmashauri ya wilaya ya Tarime kuacha tabia ya kufanyakazi kwa mazoea.

Ameyasema hayo mapema hii leo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa halmashauri hizo mbili wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani Tarime mkoani Mara ambapo ametembelea miradi ya afya, elimu, daraja na ujenzi wa nyumba za watumishi.

Aidha, Jafo amewaagiza viongozi wa halmashauri hizo mbili kukaa na kufanya maamuzi ya majengo ya halmashauri ya wilaya ya Tarime yaliyopo ndani ya eneo la halmashauri ya mji yatumike kwa matumizi ya kiofisi ya halmashauri ya mji.

Hata hivyo, ameongeza kuwa fedha zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa halmashauri ya mji zihamishiwe halmashauri ya wilaya ili waende kuanza ujenzi wa ofisini katika eneo lao badala ya kukaa ndani ya eneo la  halmashauri mji.

 

Polisi wamsaka Rais wa zamani wa Malawi kwa utakatishaji fedha
Wake India wapigwa marufuku kuita majina ya waume zao