Waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Mhe.Selemani Jafo amewataka waamuzi watakaochezesha mashindano hayo pamoja na yale ya UMITASHUMTA kuhakikisha kuwa wanachezesha michezo hiyo kwa kuzingatia kanuni na sheria bila kuwepo upendeleo ili washindi wa michezo yote wapatikane kwa haki.
Waziri Jafo ameyasema hayo leo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam ambapo amewataka amewataka wakuu wa mikoa kuhakikisha kuwa mikoa yao inapeleka wachezaji wanafunzi watakaoshiriki mashindano ya UMISSETA iliyoanza leo katika viwanja vya chuo cha Ualimu Butimba kilichopo jijini Mwanza.
Mashindano ya umoja wa michezo ya shule za sekondari Tanzania (UMISSETA) yaliyoanza leo yataendelea hadi hadi Juni 15 mwaka huu na yatafuatiwa na michezo ya UMITASHUMTA ambayo itafanyika katika viwanja hivyo hivyo kuanzia tarehe 17 juni 2018 hadi tarehe 29 juni 2018.
Michezo itakayochezwa katika mashindano ya UMISSETA ni pamoja na soka kwa wavulana na wasichana, netiboli kwa wasichana, wavu kwa wasichana na wavulana, mpira wa mikoni, mpira wa kikapu, riadha maalumu(watu wenye ulimavu), riadha ya kawaida, mchezo wa bao kwa wavulana, sanaa za maonyesho (kwaya, ngoma, mashairi, ngonjera) na mpira wa meza.

Gereza lavamiwa, wafungwa 189 watoroka
Pep Guardiola afungiwa Ulaya