Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo amewataka wahandisi washauri wanaosimamia miradi ya barabara katika maeneo mbalimbali nchini kuwa upande wa Serikali ili kudhibiti ubora wa barabara zinazoendelea kujengwa.

JAfo amesema hayo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara zinazojengwa katika jiji la Arusha kupitia mradi wa Mpango Mji Mkakati (TSCP) ‘Tanzania Strategic Cities Project’ unaosimamiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Amesema kuwa Mhandisi Mshauri anapaswa kusimama na Serikali na kutoa ushauri wenye tija utakaoleta matokeo chanya katika utekelezaji wa miradi  badala ya kuwatetea wamiliki wa kampuni zinazojenga miundombinu hiyo.

‘Serikali imetoa  hela nyingi kwa ajili ya kuwekeza kwenye maendeleo hususani miundombinu ya barabara, hivyo ni vyema sasa wataalam washauri mkawa bega kwa bega na Serikali ili kuepusha hasara inayoweza kujitokeza huko mbeleni endapo miradi hii isipojengwa kwa kiwango,” amesema Jafo

Aidha, amesema kuwa hajaridhishwa na hali ya uchafuzi wa mazingira kwenye mitaro mbalimbali ya jiji la Arusha na kuagiza mitaro hiyo ifanyiwe usafi wa mara kwa mara ili kuhakikisha jiji linakuwa safi na barabara zinazoendelea kujengwa zinadumu kwa muda mrefu.

Hata hivyo, uongozi wa jiji hilo umetakiwa kuunda makundi ya wakinamama ambao wapo tayari kufanya usafi ili kila kikundi kikabidhiwe barabara ambayo wataifanyia usafi na kutunza mazingira  huku wakipata kipato ambacho kitawasaidia kujikwamua kiuchumi.

 

Breaking News: Waitara atetea Ubunge wake, atangazwa kuwa mshindi Ukonga
Arusha kuanzisha mahakama ya jiji, yatenga milioni 20

Comments

comments