Jaji wa Mahakama ya juu nchini Mexico aliyewahi kusikiliza kesi za mabilionea wa dawa za kulevya nchini humo ikiwemo ya Joaquin Guzman maarufu kama ‘El Chapo’ ameuawa kwa kupigwa risasi kichwani nyumbani kwake.

Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi wa Mexico, Jaji Vicente Bermudez aliyekuwa na umri wa miaka 37, alipigwa risasi jana alipokuwa akitoka nje ya nyumba yake huko Metepec, umbali wa maili 43 kutoka katika mji mkuu wa Mexico, Mexico City.

Imeripotiwa kuwa Jaji huyo alikimbizwa katika hospitali ya karibu kwa gari maalum la wagonjwa lakini alipoteza maisha muda mfupi baada ya kuwekwa ndani ya gari hilo.

Hivi sasa El Chapo amefungwa katika jela yenye ulinzi mkali katika eneo lililo karibu na mpaka wa Texas, baada ya kutoroka mara mbili katika magereza yalikuwa na ulinzi mkali.

 

Je, wajua Mwalimu Nyerere ndiye chanzo China kujulikana Kimataifa? Haya hapa mambo 18 mazito
Yanga Yawasili Mwanza, Kulikabili Toto Lake Kesho