Jaji wa Oklahoma nchini Marekani, Wallace Coppedge anakabiliwa na shinikizo la kuondolewa katika nafasi yake kufuatia uamuzi wake wa kutomfunga jela mbakaji wa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 13 kwa sababu ni ‘kipofu’.

Jaji huyo alitoa hukumu ya kumuweka katika kipindi cha majaribio cha miaka 15 bila kwenda jela, Benjamin Lawrence Petty ambaye alikutwa na hatia ya kumbaka mtoto huyo mwaka 2016.

Katika ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo, Petty alimdanganya mtoto huyo kuwa amemletea zawadi ambayo iko chumbani kwake, lakini walipofika chumbani alimbaka na kumuingilia kinyume na maumbile.

Msemaji wa taasisi ya Care2, Julie Matrine ameiambia KFOR kuwa tayari wamekusanya zaidi ya sahihi 61,000 lengo ni kupata 65,000.

“Hii ni moja kati ya habari ambazo zimewachukiza watu, kwahiyo tunaendesha kampeni hii. Hii inaonesha kuwa watu duniani kote wanataka kuona haki,” alisema Matrine.

Amesema kuwa lengo hilo kuhakikisha Jaji huyo anaondolewa kwenye nafasi yake kwani sababu ya mtu kuwa mlemavu haizuii kupewa hukumu aliyostahili kutokana na kitendo cha kumuingilia mtoto kinyume cha maumbile.

Mawaziri 6 wawekwa kikaangoni bungeni
LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Februari 9, 2018