Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva amewaonya wanasiasa wanaotumia muda mwingi kutoa maneno yenye ukakasi na yaliyo kinyume na sheria ya Uchaguzi mkuu.

Jaji Lubuva amevionya vyama vyote vinavyotumia maneno hayo badala ya kunadi sera za vyama vyao na kueleza kuwa Tume itachukua hatua kali dhidi ya vyama vinavyofanya hivyo.

Kauli hiyo ya Jaji Lubuva imekuja zikiwa zimebaki takribani siku 27 kabla watanzania hawajapiga kura kumchagua rais, wabunge na madiwani huku joto likizidi kupanda. Wanasiasa wengi wameshuhudiwa wakitoa maneo makali dhidi ya wagombea wa vyama vingine hali inayotafsiriwa kuwa kinyume na utamaduni wa Tanzania pamoja na sheria za nchi.

Pacquiao Ruhsa Kurejea Ulingoni
Shamsa Ford Azikataa Fedha Za Chama...