Waombolezaji mbalimbali wakiwemo baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wamejitokeza kutoa pole nyumbani kwa aliyekuwa mwanasheria mkuu wa tanzania, Jaji Mark Bomani aliyefariki jana September 10, 2020.

Akizungumza kwa niaba ya familia, Balozi Mstaafu Juma amesema marehemu ameugua kwa muda mrefu na kupata matibabu katika hospitali mbalimbali ndani na nje ya nchi hadi umauti ulipomkuta akipatiwa matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mwili wa marehemu Jaji Bomani utazikwa September 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Bomani alizaliwa kisiwani Pemba tarehe 22 Oktoba 1943, na alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Tanzania kuanzia 1965 hadi 1976.

Uganda kufungua anga rasmi
Vichwa vikubwa kuhusishwa na ushirikina