Jaji Mkuu wa Tanzan, Mohammed Chande Othman amesema sheria ya mitandao ilipitishwa kwa lengo jema la kulinda watumiaji, wanajamii na usalama wa Taifa la Tanzania.

Jaji Mkuu, Othman Mohamed Chande

Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman

Akizungumza Jumamosi iliyopita na Watanzania waishio jijini London nchini Uingereza, Jaji Mkuu alisema kuwa takwimu zinaoenesha kati ya watanzania milioni 45, watu milioni 35 wanamiliki simu. Hivyo, kuna umuhimu wa kuwepo sheria inayotoa muongozo.

Alisema kuwa sheria hiyo imezingatia uhuru wa kutoa maoni na kupata taarifa lakini pia mipaka ya uhuru unaotolewa kama ilivyoainishwa katika ibara ya 30(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Sheria hii inakupa uhuru wa kutumia mtandao kumlinda mwanajamii wenzako. Hapa Uingereza nimeongea na mwendesha mashtaka mkuu ambaye aliniambia kuwa asilimia 60 ya makosa yanayofanyika chini ya sheria ya makosa ya kujamiiana (Sexual Offence Act) yanatokana na mitandao,” alisema Jaji Mkuu.

Jaji Mkuu alikuwa jijini London na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga, ambapo walihudhuria mkutano wa kimataifa wa kupambana na rushwa.

Kwa upande wake Balozi Mahiga, alisema kuwa dunia inabadilika kutokana na kukokana kwa utawala bora, changamoto za magaidi, biashara ya dawa za kulevya, biashara haramu ya kusafirisha binadamu na uwepo wa rushwa na ufisadi.

Balozi Mahiga alisema kuwa zamani mambo haya hayakuwa na mahali pa kuyazungumzia kwa pamoja, hivyo mkutano wa mkubwa kama ule utakuwa na tija na kusaidia kukabili tatizo hilo.

Mpinzani wa Rais Museveni apigwa rungu la 'uhaini' mahakamani
Serikali yatangaza msako wa waliokula fedha za watumishi hewa

Comments

comments