Jaji mkuu wa Marekani, John Roberts amepuuza shutuma za Rais Donald Trump dhidi ya jaji aliyeamuru baadhi ya wahamiaji wasifukuzwe nchini Marekani. huku Trump akimuita jaji huyo kuwa ni wa Obama.

Katika taarifa yake iliyotolewa na mahakama ya juu kwa vyombo vya habari vya Marekani Jaji mkuu, Roberts amesema kuwa hakuna majaji wa Obama, hakuna ma jaji wa Bush au wa Clinton, akizungumzia marais watangulizi wa Trump.

“Tunao majaji wazuri sana ambao wanafanya kazi kwa kuhakikisha kwamba kila mwananchi anayefika mbele yao mahakamani, anatendewa haki,” amesema Jaji Roberts.

Aidha, Trump amemjibu jaji mkuu wa nchi hiyo kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa twitter: “samahani Jaji Mkuu John Roberts, hakika wapo majaji wa Obama, na mara nyingi maamuzi wanayoyachukuwa ni tofauti ya raia wenye jukumu la kuzingatia usalama wa nchi yetu.”

Taarifa hiyo ya Jaji Roberts imewashangaza wengi wakisema si jambo la kawaida kwa jaji mkuu kutoa jibu la moja kwa moja kwa rais.

Hata hivyo, Jaji Roberts ndiye alimuapisha Trump alipochukua rasmi hatamu za uongozi mwaka jana.

Niliamua kukaa kimya kwa muda wa miaka mitatu- Ester Bulaya
Amuua mpenzi wake na kumfanya kitoweo