Jaji Mkuu wa Zambia, Irene Chirwa Mambilima amefariki dunia baada ya kuugua akiwa nchini Misri ambako alisafiri kikazi.

Jaji Mambilima amefariki wakati taifa hilo likiwa katika mambolezo baada ya kuondokewa na muasisi wa Taifa hilo, Hayati Dk. Kenneth Kaunda aliyefariki dunia Juni 17, 2021.

Taarifa iliyotolewa jana na Dk. Simon Miti ambaye Katibu wa Baraza la Mawaziri / Katibu Mkuu wa Rais imeeleza kuwa:

“Ni kwa masikitiko makubwa na huzuni kwamba Mheshimiwa Dk. Edgar Chagwa Lungu, Rais wa Jamhuri ya Zambia anangaza kwa taifa, kifo cha Jaji Irene Chirwa Mambilima, Jaji Mkuu wa Zambia kilichotokea Juni 20, 2021 saa 11:00 alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya binafsi Mjini Cairo, Misri,”imeeleza taarifa hiyo.

Ukarabati viwanja fursa kwa vijana
Olympic Japan: Kocha wa timu ya Uganda akutwa na Corona