Amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo ofisini kwake jijini Dar es salaam,na kuongeza kuwa  Mchakato wa kufutia usajili wa kudumu wa vyama hivyo unatokana na zoezi la uhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa mengine ya kisheria ya vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu uliofanyika kuanzia June 26, mpaka July 26, 2016.

Aidha, Mutungi amesema baaada ya kumaliza zoezi hilo la uhakiki ilibainika kuwa, vyama vya siasa hivyo vitatu vimepoteza sifa za usajili wa kudumu kwa kukiuka masharti ya sheria ya vyama vya siasa, hivyo kila chama kilipewa taarifa ya nia ya msajili kufuta usajili wake wa kudumu na kutakiwa kujieleza kwa nini visifutiwe.

Hata hivyo, Mutungi ameongeza kuwa katika utetezi wao vyama hivyo vilishindwa kutoa sababu za kuridhisha na za msingi kuwa havijakiuka sheria na bado vinazo sifa za usajili wa kudumu.

TRA yakusanya shil.trilion 1.15 kwa mwezi Oktoba
Maofisa Wa TFF Wapandishwa Kizimbani Kwa Tuhuma Za Rushwa