Msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania Jaji Francis Mutungi amekionya chama cha upinzani CHADEMA kwa kukiuka katiba na sheria za nchi kwa kuongeza aya ya tatu katika wimbo wa Taifa.

Ameyasema hayo leo Oktoba 4, 2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

“Kwa hili lililofanyika ni kama kunajisi wimbo wa taifa, Naamini kuna taasisi inahusika iko ndani ya wizara ya mambo ya ndani naamini hawawezi kukurupuka kuchukua hatua wanafuatilia jambo hili”Amesema Jaji Mutungi.

Aidha Jaji Mutungi ameitaka CHADEMA kufanya Mkutano wake Mkuu leo kwa amani na kuepuka vitendo vitakavyovunja sheria ya nchi hasa kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa Urais, Ubunge na Udiwani utakao fanyika agosti 28,2020.

Pedro afanyiwa upasuaji
Matola afichua siri ya kutwaa ASFC