Mahakama ya Juu zaidi nchini China imemteua Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Uganda, Bart Katureebe, kama mwanachama wa jopokazi la wataalamu wa kuamua mizozo ya biashara ya kimataifa.

Jaji Katureebe ambaye alistaafu kutoka Mahakama ya juu zaidi ya Uganda mwezi Juni baada ya kutimiza miaka 70 kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo, atahudumu katika kamati hiyo kwa kipindi cha miaka mine ijayo.

 “Nimefurahia sana uteuzi huu kwa sababu ni Kamati ya ngazi ya juu ambayo itaimarisha taaluma yangu,” alinukuliwa na akisema katika taarifa iliyowekwa katika mtandao wa Twitter wa Idara ya Mahakama ya Uganda huku Chama cha Mawakili nchini Uganda pia kimempongeza Jaji Katureebe.

China waliandika: “Chinese Supreme Court hires Chief Justice Emeritus Bart Magunda Katureebe as a member of its Expert Committee on adjudication of international commercial disputes for the next four years.”

Kamati hiyo ya wataalamu, iliyobuniwa mwezi Agosti, 2018,  ni sehemu ya mahakama ya Kimataifa ya Biashara ya China (CICC) ambayo ni kitengo cha mahakama ya juu zaidi ya China.

Taarifa kutoka Idara ya Mahakama ya Uganda, iliongeza kuwa kamati hiyo inayotatua mizozo ya kimataifa ya bishara inayopewa, kutoa maoni ya kisheria kuhusu Sheria ya Kimatafa wakati inapoombwa kufanya hivyo na kutoa ushauri kuhusu hatma ya baadaye ya CICC, inajumuisha viongozi 31 wa mashirika ya kimataifa, wataalamu wa sheria, wanazuoni, majaji na mawakili walioteuliwa kutoka nchi tofauti.

Ubalozi wa China nchini Uganda umempongeza Jaji Katureebe kufuatia uteuzi wake.

KMC FC safarini Morogoro kuikabili Mtibwa Sugar
Bocco, Mkwasa waibuka vinara VPL