Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga amesema jalada la kesi ya aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini limefungwa rasmi  baada ya kushindwa kubaini aliyehusika na mauaji na tayari askari waliokuwa wanashikiliwa kwa kesi hiyo wameachiwa huru kwa kuwa hawana hatia.

Biswali amesema hayo leo Aprili 20, 2018, Ikulu jijini Dar es Salaam pindi alipozungumza na waandishi wa habari huku akionya watu wanaovunjua amani kutofumbiwa macho wakiwamo waandishi wa habari.

”Katika maandamano yale ya watu zaidi ya 200, huwezi kubaini nani amehusika na kumpiga risasi Akwilina na mwili wake haukutolewa risasi yoyote na kama jalada nimelifunga, kwa hiyo askari wale nao waliokuwa wanashikiliwa wameachia huru hawana hatia.” Amesema Biswalo.

Amesema jeshi la polisi linapotumia nguvu kuzuia maandamano, haliwezi kushtakiwa au hata kukitokea vurugu na kusababisha mauaji huwezi kulishtaki jeshi.

Aidha Mkurugenzi amesema moja ya jukumu lake ni kuhakikisha amani inakwepo, hivyo ameonya vikali vyombo vya habari vinavyoweza kuchangia uvunjifu wa amani na kudai kuwa hatua kali itachukuliwa, amevitaka kuwa makini na kutimiza wajibu wao kwa kufuata misingi ya taaluma yao.

”Na niseme tu kuwa, mimi sina chama cha siasa, si mwanasiasa, kwa hiyo sitamvumilia mtu awe mkubwa wala mdogo, nitamshughulikia” amesema Biswalo

Pia ameonya wote wenye mpango wa kufanya maandamano na amesema ”waambieni wasifanye hivyo kwani wakiandamana watakwenda kuwasilimulia familia yake amesisitiza Biswalo

Breaking News: Masogange afariki dunia
Bunge kumhoji Mugabe kuhusu utata upotevu mabilioni ya Almasi