Rais wa Shirikisho la soka nchini (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za pongezi Rais mpya wa Shirikisho la soka nchini Botswana Maclean Letshwiti aliyechaguliwa kushika wadhifa huo katika uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Maclean Letshwiti ambaye ni nguli katika masuala ya biashara, alimshinda Tebogo Sebego kwa kura 32 kwa 28.

Katika barua yake ya pongezi kwenda kwa Letshwiti, Rais Malinzi amemtakia kila la kheri Rais huyo mpya wa BFA aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Mochudi Centre Chiefs maarufu kwa jina la Magosi.

Katika barua hiyo, Malinzi amesema: “Nakuandikia barua hii kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya TFF na kwa niaba yangu mwenyewe, kukupongeza wewe baada ya kushinda nafasi ya urais katika uchaguzi wa Chama cha soka nchini Bostwana.”

“Mheshimiwa Rais, uchaguzi wenu ni ushahidi tosha wa kazi nzuri iliyowapa imani katika klabu uliyoiongoza na shirikisho la soka hapo Bostwana.,” amesema Malinzi katika taarifa yake na kuahidi ushirikiano wa kutosha kwa Rais Letshwiti.

Kadhalika, Rais Malinzi aliwapongeza Segolame Ramotlhwa na Marslow Motlogelwa waliochaguliwa kuwa Makamu Rais wa Kwanza na Makamu Rais wa Pili kwa kufuatana.

Video: Hapi kumsimamisha Mganga Mkuu Mfawidhi Hospitali ya Mwananyamala
TFF Yatibua Uchaguzi Wa Chama Cha Soka Dar es salaam (DRFA)