Raisi wa shirikisho la soka nchini TFF, Jamal Malinzi ameendelea kuonyesha msisitizo katika sakata la upangaji wa matokeo ambalo limepelekwa katika kamati ya nidhamu baada ya kujadiliwa na kamati ya saa 72.

Jamal Malinzi ameendelea kuonyesha hali hiyo, hata kwa njia ya simu za mkononi kwa kutuma ujumbe kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp ambapo baadhi ya walio kwenye kundi lililomjumuisha kiongozi huyo wa soka wamediriki kuueneza katika makundi mengine.

Ujumbe wa Malinzi unasomeka kama ifuatavyo.

Salam aleikum,Hili la ligi daraja la kwanza kundi C ndugu zangu tulichukulie kwa umakini mkubwa sana.Hatua ya mwanzo maamuzi yake yaliegamia kwenye kanuni za ligi (kamati ya 72hrs),hawa waliangalia taarifa za maandishi.

Sasa limehamia kwenye kikao cha kisheria (judicial body) ambayo ni kamati ya nidhamu.Hii kamati inaendeshwa kimahakama na kuongozwa na disciplinary code ambayo ni zao la FIFA.

Hii code sio mchezo kuna life ban mle (actualy kimpira kupanga matokeo ni kama murder case).TFF lazima tujipange vizuri tukiwa na vielelezo kamili katika kuandaa mashtaka yetu (charge sheet) maana na tunaowatuhumu sharti wapewe fursa kamili ya kutoa utetezi wao.

Subira ni muhimu sana katika jambo hili ambalo kusema kweli ni jambo kubwa sana katika historia ya mpira wetu (liliwahi kutokea mara kadhaa miaka ya nyuma).Tuwape nafasi ya kutosha wanasheria wetu wajipange.” Jamal Malinzi

Chama la Wana Lajinasibu Kurejesha Heshima Nyumbani
Jibu La Nani Mbabe Dhidi Ya Mwenzake Kupatikana Kesho