Klabu ya Raja Club Athletic ya Morocco imemtimua Kocha Jamal Salami kufuatia kipigo cha 2-0 dhidi ya wapinzani wao Wydad Athletic Club kwenye Casablanca Derby iliyochezwa mwishoni mwa juma lililopita (Jumamosi –Machi 20).

Raja kwa sasa wako nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Morocco “Botola Pro” kwa alama tatu nyuma ya Wydad ambao wana mchezo mmoja mkononi.

Kocha Huyo pia kaiongoza Klabu hiyo Kufuzu Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika na Sasa wanaongoza Kundi D kwa Alama Sita sawa Pyramids FC ya Misri wakiongoza kwa magoli mengi ya Kufunga; Kundi Hilo pia zimo Nkana FC ya Zambia na Namungo FC ya Tanzania ambazo bado hazina Pointi.

Bendera ya Umoja wa Mataifa kupepea nusu mlingoti kumuenzi Magufuli
Chad yafutwa AFCON 2021