Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Upande wa mashtaka katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, wamefunga ushahidi wao bada ya kuwaita mashahidi watatu.

Wamefunga ushahidi wao leo Ijumaa Septemba 24, 2021 ambapo sasa shahidi wa kwanza katika kesi hiyo ndogo ambaye ni mshtakiwa wa pili Adam Samia Kasekwa anatarajia kuanza kujitetea.

Aidha, Mawakili wa utetezi waliyapinga yasipokelewe Mahakamani kama kielelezo cha usahidi wa upande wa mashtaka wakidai kuwa kabla na wakati wa kuyatoa maelezo hayo mshtakiwa huyo aliteswa.

Walidai pia maelezo hayo yalichukuliwa nje ya muda unaoruhusiwa kisheria.

Vibanda vilivyopo juu ya mitaro viondolewe - Rc Makalla
Mwandishi wa habari wa ITV afariki dunia