Serikali imewaongezea mashatka watuhumiwa wa Ecsrow, Mwenyekiti wa Mtendaji wa Kampuni ya Independent Power Limited/PAP, Habinder Seth Sigh na mwenzake wa Kampuni ya VIP Engenering na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL, James Rugemalira.

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka mapya sita pamoja na uhujumu uchumi na wakili wa Serikali, Patrict Mwita mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Huruma Shahidi.

Kesi hiyo itatajwa tena Julai 14, 2017.

Awali vinara hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam Juni 19, 2017 na kusomewa mashtaka sita yakiwamo ya uhujumu uchumi.

Watuhumiwa hao pia wanadaiwa kula njama, kughushi, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kuisababisha  serikali hasara ya Dola za Marekani 22, 198,544.60  (Sh bilioni 309.5).

Washtakiwa hao wote walisomewa mashtaka yao na Mwendesha Mashtaka, Wakili wa Serikali, Paul Kadushi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Washtakiwa walirudishwa rumande hadi leo Julai 3, 2017 kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza wala kutoa dhamana kwa kesi ya uhujumu uchumi.

Inadaiwa kuwa kati ya Oktoba 18 , mwaka 2011 na Machi 19 , 2014   Dar es Salaam, watuhumiwa walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Imedaiwa kuwa katika shtaka la kujihusisha na mtandao, washtakiwa hao kati ya Oktoba 18,  mwaka 2011na Machi 19, 2014   Dar es Salaam wakiwa siyo watumishi wa umma na wakisaidiana na watumishi wa umma, walitekeleza mtandao huo wa uhalifu kwa lengo la kujipatia faida.

Katika shtaka la nne mtuhumiwa Sethi anadaiwa kuwa Oktoba 10, 2011 katika Mtaa wa Ohio Ilala Dar es Salaam akiwa na nia ya ulaghai alighushi fomu namba 14 ya usajili wa makampuni na kuonyesha yeye ni Mtanzania anayeishi Kitalu namba 887 Mtaa wa Mrikau Masaki wakati akijua si kweli.

 

Seth anadaiwa kutoa nyaraka hiyo ya usajili wa Kampuni kwa Ofisa Msajili wa Makampuni, Seka Kasera kwa njia ya kuonyesha kwamba yeye ni Mtanzania na mkazi wa Mtaa wa Mrikau.

Katika shtaka jingine, washtakiwa wote, wanadaiwa kuwa kati ya Novemba 28/29, 2011 na Januari 23, 2014 makao makuu ya Benki ya Stanbic Kinondoni na Benki ya Mkombozi Tawi St. Joseph kwa ulaghai, walijipatia kutoka Benji Kuu ya Tanzania  (BOT), Dola za Marekani 22,198,544.60  (zaidi ya Sh bilioni 309.5).

Ilidaiwa  kuwa katika shtaka la kusababisha hasara, washtakiwa hao wanadaiwa  Novemba 29, mwaka 2013 katika Benki ya Stanbic Tawi la  Kinondoni, kwa vitendo vyao, waliisababishia Serikali hasara ya USD 22, 198, 544.60 na Sh bilioni 309.5.

Baada ya kumaliza kusomewa mashtaka yao, Wakili wa utetezi,  Respicius Didas kwa niaba ya mawakili wenzao, aliomba mahakama iwapatie wateja wao dhamana kwa sababu mashtaka yanayowakabili yanadhaminika.

Upande wa mashtaka ulipinga vikali hoja hizo na kuiomba mahakama kutupilia mbali maombi ya utetezi ya kuwapatia dhamana washtakiwa hao.

Akiwasilisha hoja zake, Wakili Kadushi alisema mahakama ya Kisutu haina mamlaka si tu ya kutoa dhamana, bali hata kusikiliza maombi ya dhamana.

Alisema mahakama pekee yenye mamlaka ya kufanya hivyo ni Mahakama Kuu na ndiyo maana washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote wakati wakisomewa mashtaka yao.

Wakili huyo wa Serikali alisema mazingira pekee ambayo yangeifanya Mahakama ya Kisutu iweze kusikiliza maombi hayo na kesi kwa ujumla ni pale ambako Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) angetoa cheti maalum cha kuipa mamlaka Mahakama ya Kisutu kuisikiliza kesi hiyo.

“Maombi ya dhamana yameletwa katika mahakama isiyoweza kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria,” alisema Kadushi.

Naye Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi alisisitiza na kuiomba mahakama kutupilia mbali hoja zote za maombi ya dhamana zilizotolewa na upande wa utetezi na ijielekeze kwa jinsi inavyoona inafaa, washtakiwa waende mahabusu wakati wakisubiri taratibu za kesi zinazoendelea.

Akijibu hoja hizo, Hakimu Shaidi alisema sheria inaelekeza kwamba kesi za uhujumu uchumi zinazozidi Sh milioni 10 Mahakama hiyo haina mamlaka ya kuisikiliza wala kutoa dhamana isipokuwa kwa cheti maalumu kutoka kwa Mwendesha Mashataka wa Serikali (DPP),  kinachoiwezesha mahakama kufanya hivyo.

?Live: Majadiliano ya Kamati ya bunge kuhusu marekebisho ya sheria ya Madini
?Live: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Julai 3, 2017