Mshambuliaji wa klabu bingwa nchini England, Leicester City, Jamie Vardy amevunja ukimya na kuanika wazi mustakabali wa soka lake kwa msimu ujao wa 2016-17.

Vardy alikua amewaweka njia panda mashabiki wa soka duniani, kufuatia sakata la kushindwa kusema ni wapi atakapocheza msimu wa 2016-17, baada ya Arsenal kuwasilisha ofa ya kutaka kumsajili, amekubali kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuituimikia Leicester City.

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu ya Leicester City, zinaeleza kwamba, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29, atasaini mkataba mpya wa miaka minne ambao utamuwezesha kulipwa mshahara wa Pauni 120,000, tofauti la ule wa sasa ambao unampa wigo wa kulipwa Pauni 100,000 kwa juma.

Siku kadhaa baada ya Arsenal kuwasilisha ofa ya kutaka kumsajili Vardy kwa ada ya Pauni milioni 20, mshambuliaji huyo alishindwa kutangaza msimamo wake na akaahidi kufanya hivyo mara baada ya fainali za Euro 2016 zinazoendelea nchini Ufaransa.

Diamond Platinumz kuwa ‘mgeni Muhimu’ ndani ya E! Entertainment
Rangers Wakamilisha Usajili Wa Niko Kranjcar