Hatimaye Kiongozi wa muda mrefu nchini Gambia Yahya Jammeh, amesema kuwa ataondoka madarakani baada ya kukataa kukubali kushindwa.

Katika tangazo hilo lililo tolewa kwenye televisheni ya taifa ya Gambia, Jammeh amesema kuwa hakuna haja ya kumwaga hata tone moja la damu kwa wanajeshi au kwa wananchi sababu ya kugombea madaraka.

Aidha, Tangazo hilo limekuja saa chache  baada ya mazungumzo kati ya Jammeh na wapatanishi wa Afrika Magharibi. lakini hata hivyo hakuna taarifa zaidi kuhusu yale yaliyofikiwa katika mazungumzo hayo.

Jammeh alishindwa kwenye uchaguzi wa mkuu wa urais uliofanyika mwezi Disemba na mrithi wake Adama Barrow ambaye tayari ameshaapishwa katika ubalozi wa Gambia nchini Senegal, aidha Mpaka sasa  Barrow anaishi nchi jirani ya Senegal kwa siku kadhaa.

Nchi za mbalimbali Afrika Magharibi ikiwemo Senegal zimetuma majeshi nchini Gambia kwajili ya kumng’oa madarakani Jammeh.

Hata hivyo, Uamuzi wa Jammeh kuondoka umekuja mara baada ya kufanya mazungumzo na marais wa Guinea na Mauritania.

Lipumba awananga Chadema,asema ni waroho wa madaraka
Video: Rais Tayyip Erdogan wa Uturuki kutembelea Tanzania