Zaidi ya dola za Kimarekani milioni 11 zimetajwa kupotea katika hazina ya Serikali ya Gambia kufuatia kuondoka madarakani kwa mtawala wa muda mrefu Yahya Jammeh.

Taarifa hizo zimetolewa na Ahmad Fatty, mshauri maalumu wa Rais wa sasa wa Gambia, Adama Barrow alipoongea na Waandishi wa habari katika mji mkuu wa Senegal Dakar kwamba wataalamu wa masuala ya fedha wanatathmini kujua ni kiasi gani kwa sasa kimepotea.

Ahmad Fatty amesema kuwa kwa sasa Gambia ina tatizo kubwa kifedha kwa hazina yake kutokuwa na kitu.

Rais Barrow amekuwa akifanya kazi na timu ya wataalamu wa masuala ya fedha na wengine kutoka Benki kuu ya nchi hiyo kupata kiasi halisi kilichopo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Gambia, magari ya kifahari na mali nyingine zilionekana zikipakiwa katika ndege ya mizigo ya Chad kwa niaba ya Rais Jammeh siku alipoondoka nchini humo.

Aidha, katika Ikulu ya nchi hiyo jana jioni majeshi ya Senegal yameingia kwa ajili ya kuweka usalama kabla ya kurejea nchini kwa Adama Barrow.

Yaya Toure: Andre Marriner Hakututendea Haki
Claudio Ranieri Akubali Kubebeshwa Mzigo Wa Lawama