Hatimaye Aliyekuwa rais wa Gambia Yahya Jammeh  amekubali kuachia madaraka na kuamua kwenda kuishi uhamishoni katika nchi ya Equtorial Guinea.

Jammeh amewasili nchini Equatorial Guinea, siku moja baada ya kuachia madaraka kwa Adama Barrow, aliyemshinda katika uchaguzi wa urais mwezi Disemba mwaka jana.

Aidha,Jammeh amesafiri kwa ndege kutoka Banjul hadi Guinea bila kutoa taarifa kwa mtu yeyote na baadaye kuendelea na safari yake kwenda Equatorial Guinea, aidha Jana Jammeh alitangaza ataachia madaraka baada ya kuiongoza Gambia kwa muda wa miaka 23.

Kwa mujibu wa jumuiya ya kiuchumi ya Afrika magharibi ECOWAS, Jammeh amewasili salama nchini Equatrial Guinea na anatarajiwa kuanza maisha yake mapya huko baada ya kuiongoza Gambia kwa muda wa miaka 23.

Siku ya Alhamisi ECOWAS illituma vikosi vyake vya majeshi nchini Gambia ili viweze kutumia nguvu kumng’oa kama angegoma kuachia madaraka.

Jumuiya hiyo pia imesema imesitisha oparesheni yake ya kijeshi Gambia lakini wanajeshi elfu saba watabakia nchini humo kwaajili ya  kudumisha usalama, huku Adama Barrow akitarajiwa kurejea Gambia kutoka nchi jirani ya Senegal muda mfupi ujao.

Trump avilaumu vyombo vya habari Marekani,asema havimtendei haki
Video: Serikali yatoa sh. bilioni 1.4 ujenzi wa Hospitali Njombe