Kocha mkuu wa klabu ya Mwadui FC ya mkoani Shinyanga, Jamhuri Kiwelu Julio, amewatolea uvivu viongozi wa klabu ya Simba chini ya mwenyekiti wake Evans Aveva, kwamba wamekalia majungu na roho mbaya ndani ya klabu hiyo na ndiyo sababu ya kushindwa kufanya vizuri kwa msimu wa nne sasa.

Amesema kipindi ambacho walikuwa wanakinoa kikosi cha Simba akiwa chini ya Abdallaha King Kibaden kama kocha msaidizi, kulikuwa na ukiritimba mkubwa ndani ya klabu hiyo kiasi cha kufikia hatua ya kuwatimua wakati timu ikishikilia nafasi ya tatu kwa madai kwamba hawana msaada wowote.

Itakumbukwa kwamba baada ya Julio na Kibaden kutimuliwa Simba ikiwa inashikilia nafasi ya tatu, uongozi ukafanya makubaliano na kumleta kocha wa kigeni Logarusic, ambaye alikiongoza kikosi hicho hadi mwishoni mwa msimu na kumaliza wakiwa katika nafasi ya nne.

“Ubabaishaji, roho mbaya na ukiritimba uliopo ndani ya Simba utawafanya wazidi kuweweseka kila msimu, wewe angalkia mimi na Kibadeni walitufukuza kihuni bila hata kutulipa stahiki zetu,”

“Wakamuajiri kocha mzungu ambaye amekuja kula tu hela zao lakini hakuna chochote alichofanya, tumeiacha timu ikiwa katika nafasi ya tatu yeye kawaporomosha hadi nafasi ya nne” Alisema Julio

Klabu hiyo kongwe nchini inamaliza msimu wa nne sasa bila kuchukua ubingwa licha ya kubadilisha makocha kadhaa wa ndani na wale wa kigeni.

Lissu achafua hali ya hewa Bungeni, aivaa serikali na 'Hapa Kazi Tu'
GD Sagrada Esperanca Wawasili Dar es salaam