Tottenham wanajiandaa kupambana katika michezo ya kimashindano inayowakabili kwa sasa, bila ya kuwa na beki kutoka nchini Ubelgiji Jan Vertonghen kwa kipindi cha majuma kadhaa yajayo.

Spurs, wamethibitisha taarifa za kutokuwepo kwa beki huyo mwenye umri wa miaka 28, baada ya kubainika aliumia vibaya goti la mguu wake wa kuliwa wakati wa mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England dhidi ya Crystal Palace.

“Madaktari wetu wataendelea na kazi ya kumuangalia kwa ukaribu, na tunaamini ataweza kurejea tena uwanjani kusaidiana na wachezjai wengine katika mapambano ya kufikia lengo tulilojipangia msimu huu.” Ni taarifa ya Spurs ambayo imeainishwa katika tovuti ya klabu.

Embedded image permalinkJan Vertonghen akitolewa nje ya uwanja wakati wa mchezo dhidi ya Crystal Palace

Vertonghen, alipatwa na majeraha ya goti baada ya kugongana na Connor Wickham, katika mchezo ambao ulimalizika kwa Crystal Palace kukubali kufungwa mabao matatu kwa moja.

Hata hivyo hofu iliyotanda klabuni hapo ni kwamba huenda Vertonghen akakaa nje ya uwanja kwa kipindi cha majuma 12.

Mwesigwa Afungua Kozi Ya Ngazi Ya Juu Kwa Wanawake
16 Bora Ya Kombe La FA Yazidi Kupendeza