Jangili mmoja nchini Marekani ameamriwa kuangalia filamu ya wanyama ya Bambi kila mwezi baada ya kukutwa na hatia ya kuua mamia ya mbawala.

Muwindaji huyo kutoka Missouri nchini humo, David Berry Jr anatakiwa kuangalia filamu hiyo walau mara moja kwa mwezi wakati akitumikia kifungo chake cha mwaka mmoja gerezani.

Berry alitiwa mbaroni mwezi Agosti pamoja na ndugu zake wawili kwa kuwaua mbawala, kisha kuwachinja na kuondoka na vichwa huku akiacha miili ya wanyama hao ioze, waendesha mashtaka wamesema.

Aidha, uchunguzi uliofanyika kwa muda wa miezi kadhaa kwenye majimbo kadhaa ulipelekea kunaswa kwa Berry Jr, baba yake David Berry Sr na kaka yake Kyle Berry, limeripoti gazeti la the Springfield News-Leader.

Hata hivyo, taarifa zinasema kuwa Kesi hiyo ni moja ya kesi kubwa zaidi za ujangili kuwahi kuripotiwa kwenye historia ya jimbo la Missouri.

 

Sumaye ataja ugonjwa unaoitafuna Chadema
Serikali kujenga uwanja mkubwa wa Ndege mkoani Mtwara

Comments

comments