Dogo Janja aka Janjaro amejibu swali la mashabiki wake wengi kuhusu mpango wa kujiunga na kundi la ‘Weusi’ ambalo ameonekana kuwa karibu nalo zaidi kwa siku za hivi karibuni.

Akifunguka kupitia Burudani Buzz ya Azam TV, Janjaro amesema kuwa hana mpango wa kujiunga na Weusi kwani tayari ni familia yake ambayo huzipitia nyimbo zake zote kabla ya kuziachia.

“Weusi ni watu wanao ni-support sana. Hata kabla sijatoa wimbo wangu, wao ndiyo watu wa kwanza kuusikiliza. Ni familia yangu,” alisema.

Amesema kuwa anawaheshimu sana Weusi kwa jinsi wanavyompa ushauri kwenye kazi zake za muziki hususan rapa Nikki wa Pili ambaye amekuwa na ukaribu naye zaidi.

Janjaro amewahi kuonekana mara kadhaa jukwaani akiimba na ‘Weusi’ na kurap shairi la rapa AKA kwenye wimbo wa Joh Makini ‘Don’t Bother’.

Rapa huyo kutoka Arusha yuko chini ya ‘Tip Top Connection’ ambapo Bosi wake wa karibu zaidi ni Madee.

Video: Harry Kane azidi kuing'arisha Spurs
Hemed Phd aeleza familia ‘ilivyomvuta shati’...