Timu ya taifa ya wanawake ya Japan imevuliwa ubingwa baada ya kukubali kubanjuliwa na kikosi cha Marekani katika mchezo wa hatua ya fainali kwenye michuano ya kombe la dunia uliochezwa mjini Vancouver, Canada.

Mwana dada anayeitumikia klabu ya Houston Dash ya nchini Marekani, Carli Lloyd alionekana kuwa mwiba mkali dhidi ya safu ya ulinzi ya Japan, kufutia uhodari wake wa kufunga mabao matatu ya mwanzo katika dakika ya 3, 5 na 16 kabla ya Lauren Nicole Holiday wa FC Kansas City na Tobin Powell Heath wa klabu ya Portland Thorns FC hawajaongeza bao la tatu na la nne kwenye dakika za 14 na 54.

Mabao ya kujipoza machungu kwa Japan yalipachikwa na Yuki Ogimi wa klabu ya Wolfsburg na Julie Beth Johnston wa klabu ya Chicago Red Stars aliyejifunga mwenywe.

Mbali na kunyakua taji la ubingwa wa faianli za mwaka huu, timu ya taifa ya Marekani pia imefanikiwa kumtoa mfungaji bora wa michuano hiyo, Carli Lloyd aliyepachika mabao sita pamoja kutwaa tuzo ya mchezaji bora.

Hata hivyo, katika tuzo ya ufungaji bora Loyd amefungana na Célia Šašić wa timu ya taifa ya Ujerumani ambaye pia amefunga mabao sita.

Naye mlinda mlango wa timu ya taifa ya Marekani, Hope Solo ametwaa tuzo ya kipa bora, huku tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa fainali za mwaka huu ikichukuliwa na Kadeisha Buchanan kutoka nchini Canada.

Timu iliyochukua tuzo ya nidhamu bora katika fainali za kombe la dunia kwa wanawake ni timu ya taifa ya Ufaransa.

Ikumbukwe pia timu ya taifa ya England ilifanikiwa kutwaa nafasi ya tatu baada ya kuibanjua timu ya taifa ya Ujerumani kwa bao moja bila ya majibu.

CCM: Hatutachagua Mgombea Kwa Shinikizo La Wapambe
Breaking News: Daniel Yona Na Bazil Mramba Wafungwa Jela