Wanachama kadhaa wa Simba, wametinga mahakamani na kuweka pingamizi la mkutano wa Simba uliopangwa kufanyika Jumapili.

Mkutano wa Simba, uliitishwa na uongozi wa klabu ikiwa ni kujadili masuala kadhaa likiwemo suala la mabadiliko.

Tayari mfanyabiashara bilionea, Mohammed Dewji maarufu kama Mo amesema yuko tayari kutoa Sh bilioni 20 na kuwekeza Simba.

Lakini kuna wanachama wa Simba wamekuwa wakipinga hilo ingawa idadi yao inaonekana ni ndogo sana.

Wanachama hao wamewasilisha pingamizi hilo katika mahakama ya Wilaya ya Ilala iliyopo Lumumba jijini Dar es Salaam.

Wakati huo huo Mahakama ya Wilaya ya Ilala imetupilia mbali pingamizi la baadhi ya wanachama wa klabu ya Simba waliotaka kuzuiwa kwa mkutano uliopangwa kufanyika Jumapili.

Mahakama hiyo imewaona waliopinga kuwa hawana hoja ya msingi na kupitisha mkutano huo ufanyike Jumapili.

Mkutano huo umepangwa kufanyika Jumapili kwa lengo la kujadili masuala kadhaa ya klabu hiyo likiwepo lile la mabadiliko.

Tayari mfanyabiashara bilionea, Mohammed Dewji maarufu kama Mo amesema yuko tayari kutoa Sh bilioni 20 na kuwekeza Simba.

Aliyenusurika Ajali Ya Ndege Aanza Kutembea
Azam FC Kujipima Na Mtibwa Sugar