Inaelezwa kuwa mwanamuziki maarufu kutoka nchini Marekani Jason Derulo ni mmoja wa wanamuziki wasioweza kuvumilia hata kidogo hasa inapotokea akafananishwa na msanii mwingine yeyote wa R&B.

Hilo limedhihirika baada ya Jason kuwashambulia watu wawili katika hotel moja huko Las Vegas kwa kosa la kumuita jina la msanii mwingine wa R&B ‘Usher’.

Kwa mujibu wa  TMZ, polisi waliitwa kwenye hoteli ya ARIA asubuhi ya Jumanne Desemba 4, 2022 baada ya Derulo kurusha ngumi kwa wanaume wawili waliomuita jina lisilo la kwake.

Watu walioshuhudia tukio hilo wanasema Derulo na mmoja wa wanaume hao walikuwa wakipishana kwenye ngazi ambapo kijana mmoja kati yao alionekana kumpapasa Derulo huku akipiga kelele, “Hey, Usher! huku akitamka maneno mengine yasiyo mazuri.

Na hapo ndipo Derulo alipokasirika na kumpiga ngumi ya uso moja kwa moja, iliyompeleka yule jamaa chini. Haikuishia hapo, inadaiwa Jason pia alimpiga kofi mtu wa pili muda mfupi baadaye, na askari wa usalama wakalazimika kuingilia kati ili kuzuia ghasia hizo.

Wanaume hao wawili walioshambuliwa na Derulo hawakutaka kushtaki, japo bado kuna uwezekano wa lolote kutokea kwa kuwa kwa mujibu wa sheria wana hadi mwaka mmoja wa kuamua kubadili mawazo yao ikiwa wataamua kumpeleka Jason Mahakamani au kulitupilia mbali suala hilo.

Inaelezwa Jason Derulo alitakiwa kuhama kutokana na uvunjaji sheria kutoka kwa ARIA, na akaondolewa katika eneo hilo haraka.

Vyanzo vya habari vinasema, wanaume hao wawili walionekana kumwaga damu kutokana na majeraha ya usoni waliyoyapata baada ya kipigo hicho.

Uchumi wa Tanzania Umepanda
Nchi ya Sudan yapewa onyo