Beki kutoka nchini Argentina, Javier Mascherano amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela na kupigwa faini ya Euro 815,000 kwa kukutwa na hatia mbili za kukwepa kodi.

Pamoja na hayo, nyota huyo wa Barcelona hataki kwenda kutumikia kifungo hicho jela, baada ya Mwanasheria wake, David Aineto kuomba kifungo cha jela kigeuzwe kuwa faini, ambayo tayari amelipa.

Mwanasheria wa Mascherano pia anapambana kuondoa rekodi ya ukwepaji kodi kwa mteja wake kwa kulipa faini zaidi.

Nchini Hispania watu wanaohukumiwa kifungo kisichozidi miaka miwili jela, huruhusiwa kulipa faini ili wasiende jela, labda wawe wamehukumiwa kwa makosa ya jinai.

The hearing on Thursday lasted only 10 minutes, according to reports in SpainJavier Mascherano akiwa mahakamani akisikiliza hukumu dhidi yake.

Mascherano, mwenye umri wa miaka 31, alihukumiwa kifungo cha miezi minne na miezi minane kwa makosa mawili aliyoyafanya mwaka 2011 na 2012.

Nyota huyo wa Argentina tayari amelipa kiasi cha kodi anachodaiwa kukwepa Euro Milioni 1.6 kabla ya kupewa adhabu hiyo. Mascherano pia amelipa ziada ya fedha hizo, lakini bado ametozwa faini.

Makosa yake ya ukwepaji kodi ni kutokana na kushindwa kuainisha vipato vyake vingine kutokana na haki za matumizi ya picha zake ambazo zinamilikiwa na kampuni za Ureno na Marekani.

Kikwete atunukiwa shahada ya udaktari wa falsafa
Magufuli awanyooshea kidole wakuu wa shule za msingi, sekondari