Licha ya kuzua gumzo kote ulimwenguni baada ya kurejea kujiunga na mtandao wa instagram na kupata idadi ya wafuasi zaidi ya milioni mbili ndani saa 24 Rapa Jay z ameifuta tena account yake ya mtandao wa Instagram.

Fununu zinazoendelea kuenea ni kuwa rapa huyo aliifungua account hiyo kwa ajili ya ku-promote filamu yake mpya iitwayo ‘The Harder They Fall’ na si kitu kingine, hivyo pengine kiwango cha watu aliotamani wapate taarifa za filamu hiyo kilitimia ndani ya muda mchache tangu kujiunga kwake kwenye mtandao huo kupitia post moja pekee aliyoiweka yenye kuonyesha Cover linalodaiwa kuwa la filamu hiyo.

Ndani ya masaa matatu pekee Jay z alifanikiwa kupata wafuasi zaidi ya Milioni moja, hii ikiwa imevunja rekodi yake mwenyewe ya Agosti 29, 2015 ambapo alijiunga na mtandao huo na ku-post picha moja ya marehemu Michael Jackson kwenye siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake kisha kuifuta account hiyo ndani ya masaa 14 ikiwa tayari ina jumla ya wafuasi (followers) Laki moja.

Mukoko: Nimepitia changamoto nyingi
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Novemba 4, 2021