Mwanamuziki Jay Z anaendelea kujiandikia rekodi za kipekee kwenye kiwanda cha muziki Duniani, achana na mengi yenye kumuweka kwenye nafasi ya kuwa msanii namba moja wa rap aliyefanikiwa zaidi.

Kwa sasa gumzo ni jina la msanii na mjasiriamali huyo kutajwa mara nyingi zaidi kwenye vipengele vya tuzo za Grammy muda wote.

Jay Z kwa sasa amefanikiwa kufikisha jumla ya nominations 83, ambapo ni juu ya mtayarishaji Quincy Jones mwenye umri wa miaka 80.

Hii ni kufuatia Jay Z kutajwa tena kwenye vipengele vitatu kwenye tuzo za Grammy mwaka 2022, akiingia kupitia kolabo ya ngoma iitwayo ‘Bath Salts’ aliyofanya na marehemu DMX pamoja na Jail aliyoshirikiana na Kanye West.

Kipengele kingine kinaihusu album ya Kanye West Donda ambayo Jay Z ameshiriki pia. Pamoja na hayo, mpaka sasa Hov amewahi kushinda tuzo za Grammy takrubani mara 23.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa ajiuzulu
Tyson aombwa kuwa balozi wa bangi Malawi